Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujasiri wa Bi Sahar Emami, mtangazaji wa Seda wa Sima ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wakati wa shambulizi lililofanywa na utawala wa kishetani wa Kizayuni dhidi ya jengo la media, umemgeuza kuwa mwanamke shujaa wa Kiirani.
Mtangazaji huyu jasiri na mwenye ghira, baada ya milipuko miwili iliyotokana na shambulizi la utawala wa kishetani wa Kizayuni dhidi ya jengo la media, aliendelea na kazi yake na akaanza kutoa hotuba za majigambo dhidi ya Israel.
Sahar Emami aliwahutubia watu wa Iran na kusema: “Mlio mliosikia ni sauti ya mvamizi dhidi ya sauti ya haki na ukweli.”
Ni vyema kutaja kuwa, katika kuitikia hatua ya mtangazaji huyu mwanamke jasiri, wimbi la jumbe za kujivunia kutoka kila kona ya dunia limejaa katika mitandao ya kijamii.
Maoni yako